- 264 viewsDuration: 2:44Ilikuwa imetajwa kama suluhu ya upatikanaji wa huduma ya afya kwa wakenya wote. Ila miezi kadhaa baada ya kuzinduliwa kwake, mamlaka ya afya ya jamii SHA imekumbwa na changamoto chungu nzima. Hii leo Taasisi ya maswala ya Uchumi, IEA Kenya imezindua ripoti inayoonyesha changamoto hizi na kutaja ukosefu wa ufadhili wa kutosha kama mojawapo ya maswala yanayochangia matatizo yanayoshuhudiwa katika utekelezaji wa SHA.