- 465 viewsDuration: 1:45Wakaazi wa Ndambwe Mkunumbi kaunti ya Lamu wamefanya maandamano ya kushikinikiza serikali kuwapa Naibu wa chifu ambaye ni mwenyeji na mkaazi wa eneo hilo. Hii ni baada ya Naibu wa chifu aliyekuwepo kustaafu na nafasi yake kusalia kuwa wazi .Kulingana na wakaazi hao, eneo hilo linakabiliwa na tatizo la usalama na hivyo wanakisia kuwa chifu ambaye ni mwenyeji wa eneo hilo ana ufahamu zaidi kuhusu shida zinazokabili wananchi na itakuwa rahisi kuwasiliana na maafisa wa usalama.