Skip to main content
Skip to main content

Msichana afariki baada ya kupigwa vibaya Narok

  • | Citizen TV
    3,212 views
    Duration: 1:46
    Hali ya majonzi imetanda katika Kijiji cha Emitik katika Wadi ya Sogoo eneo bunge la Narok Kusini, kufuatia kifo cha msichana wa miaka 14 baada ya kupigwa. Msichana huyo Peris Chepng’eno, ambaye ni mwanafunzi wa gredi ya saba, anadaiwa kkuzirai alipokuwa akiadhibiwa na mamake, kwa ushirikiano na dadake kufuatia makosa ya kinyumbani. Chifu wa eneo hilo Benard Bunei, amewatahadharisha wazazi kuwa na subira na kutafuta mbinu zisizowadhulumu watoto wanapowaadhibu.Wahusika wamekamatwa na wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Ololulung’a.