Skip to main content
Skip to main content

Jane Gatwiri, mamake Mwenda Mbijiwe aliyetoweka mwaka wa 2021, ataka haki ya mwanawe

  • | Citizen TV
    188 views
    Duration: 1:11
    Jane Gatwiri, mamake Mwenda Mbijiwe aliyetoweka mwaka wa 2021, ameieleza mahakama kuwa serikali inafahamu aliko mwanawe na mahali anapozuiliwa. Gatwiri anasisitiza kuwa mwanawe, mchambuzi wa masuala ya usalama, bado yuko hai, akitaka awasilishwe mahakamani. Gatwiri aliitaka mahakama imuamuru Inspekta Jenerali wa Polisi, Mkurugenzi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), pamoja na vyombo vingine vya usalama, wamfikishe mwanawe mahakamani mara moja na bila masharti yoyote. Katika hati ya kiapo, Gatwiri anaeleza kuwa Mbijiwe alitekwa nyara Juni tarehe 12, 2021, katika eneo la Roysambu jijini Nairobi, alipokuwa akisafiri kuelekea Kaunti ya Meru.