- 48,530 viewsDuration: 4:10Watu saba wameripotiwa kujeruhiwa baada ya polisi kurusha vitoa machozi kwenye mkutano wa kisiasa wa mrengo wa ODM unaoongozwa na katibu mkuu Edwin Sifuna eneo la Kitengela kaunti ya Kajiado. Mkutano huu ulitatizwa kiasi kufuatia wingu la vitoa machozi huku wanasiasa waliozungumza wakielezea uungaji mkono wao kwa Sifuna kusalia Katibu mkuu. Aidha, waliendelea kurusha makali kwa wale wanasema wameuza na kuvuruga chama cha ODM.