Inspekta generali wa polisi Japhet Koome ameapishwa leo na jaji mkuu Martha Koome

  • | K24 Video
    16 views

    Inspekta generali wa polisi Japhet Koome amewaonya maafisa wa polisi wanaohusika katika uhalifu kwamba watakabiliwa ipasavyo kufuatia mabadiliko katika idara ya polisi. Koome ambaye alikula kiapo hii leo kwenye hafla iliyoongozwa na jaji mkuu Martha Koome katika mahakama kuu, aidha ametoa onyo kwa wahalifu wanaohusika na utovu wa usalama unaoshuhudiwa kwa sasa. japhet koome ameapishwa kuwa inspekta jenerali wa nne akichukua pahala palipoachwa na Noor Gabow aliyekuwa anashikilia wadhfa huo baada ya kuondoka kwa Hillary Mutyambai.