Skip to main content
Skip to main content

Wakazi wa Kaptich wafanya maandamano wakilalamikia utapeli wa kazi Nandi

  • | Citizen TV
    216 views
    Duration: 1:59
    Wakazi wa Kaptich, katika eneo bunge la Mosop, kaunti ya Nandi walindamana wakitwataka polisi kumkamata mshukiwa mmoja aliyetapeli wakazi shilingi milioni 3 kwa ahadi za kuwapa vijana ajira za serikali. Wakazi hao walilalamikia utapeli wa mamilioni ya pesa uliotekelezwa na mtu anayefahamika vyema eneo hilo. Wakaazi hao wanadai kuwa mshukiwa alijipatia shilingi milioni tatu kutoka kwa familia moja kwa ahadi ya kuwatafutia kazi vijana sita wa familia hiyo katika idara za usalama. Familia iliyoathirika, ilifichua kuwa ililazimika kuuza kipande cha ardhi cha ekari tatu ili kupata kiasi hicho cha pesa. Licha ya mshukiwa kujaribu kujitenga na madai hayo, familia hiyo imetoa nyaraka na ujumbe wa miamala ya Mpesa inayothibitisha kutumwa kwa pesa hizo moja kwa moja kwa nambari ya mshukiwa huyo.