- 19,483 viewsDuration: 1:44Shirikisho la kandanda barani ulaya UEFA limeanzisha uchunguzi kuhusiana na tukio la nyota wa Brazil Vinicious Junior aliyeripoti kufanyiwa ubaguzi wa rangi na mchezaji wa Benfica Prestianni katika mechi ya klabu bingwa ulaya kati ya Real Madrid na Benfica. Uefa imesema baraza maalum la nidhamu na maadili limeteuliwa kufuatilia kesi hiyo na imeahidi kutoa taarifi kamili siku chache zijazo. Prestianni ambaye ni raia wa Argentina amekanusha madai hayo, huku klabu yake ikimtetea. Lakini iwapo atapatikana na hatia, huenda akakabiliwa na marufuku ya mechi 10 katika michuano ya ulaya. Ahmed Bahajj anatuarifu zaidi kuhusu tukio hilo - - #bbcswahili #vinicious #kandanda #soka #michezo Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw