Skip to main content
Skip to main content

Murkomen asema wahuni ndio waliovuruga mkutano Kitengela

  • | Citizen TV
    2,433 views
    Duration: 1:22
    Waziri wa Usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen amesema kuwa polisi hawakufahamishwa mapema kuhusu mkutano ulioongozwa na Katibu Mkuu wa ODM, Edwin Sifuna eneo la Kitengela kaunti ya Kajiado jumapili iliyopita. Murkomen amesema kuwa jambo hilo lilliwafanya washindwe kudhibiti hali ilivyotokea. Akizungumza katika eneo bunge la Naivasha kaunti ya Nakuru, Waziri huyo pia amedai kuwa wahuni walisafirishwa kutoka kaunti za Machakos na Nairobi ili kuvuruga mkutano huo. Aidha, ameeleza kuwa visa vya uchochezi wa kisiasa vimeongezeka, na akasisitiza kuwa serikali haitakubali vitendo vya kuvuruga mikutano ya kisiasa kuendelea