Wafugaji wavua samaki wakiwa wachanga kwa kuogopa watakufa

  • | Citizen TV
    420 views

    Wafugaji wa samaki katika ufuo wa Ogal kaunti ya Kisumu wanakadiria hasara ya shilingi bilioni moja, baada ya samaki wanaofugwa kizimbani kuanza kufa ovyoovyo kuanzia jumapili usiku. Kulingana na wafugaji hao, hawakutarajia hali hiyo kuwafikia, kwani vizimba vyao havikuwa karibu na ufuo ambapo mchanganyiko wa maji unafanyika. Taasisi ya utafiti ya uvuvi na ubaharia nchini ilitabiri kuwa vifo zaidi vya samaki vitaendelea hadi mwisho wa mwezi Novemba, ambapo mabadiliko ya mkondo wa upepo ziwani yatakuwa yamekamilika. Wafugaji hao sasa wanawavua samaki hao walioangamia, na kuyakausha kabla ya kuuza ili kupunguza hasara waliyopata. Vizimba zaidi ya 600 vimeathirika katika ufuo wa Ogal Kisumu, na Homa Bay