Skip to main content
Skip to main content

Makanisa yawataka wanasiasa kupunguza kelele kisiasa

  • | Citizen TV
    284 views
    Duration: 1:30
    Askofu Mkuu wa kanisa la Kianglikana nchini Jackson Ole Sapit, sasa anaitaka tume ya uchaguzi nchini kuzima kwa haraka nyuzi joto za siasa zinazoendelea kupanda, zaidi ya mwaka mmoja unusu kabla ya uchaguzi mkuu mwakani. Sapit akikemea kuongezeka kwa matumizi ya magenge katika mikutano ya kisiasa, akionya kuwa tabia hiyo inahatarisha usalama na uthabiti wa taifa. Aidha amewataka wanasiasa kuzima kelele za siasa za malumbano na kushughulikia huduma kwa wakenya .