- 22,274 viewsDuration: 7:47Ripoti kutoka mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, zinasema kuwa Msemaji wa M23, Willy Ngoma, ameuawa kwenye shambulio la ndege zisizo na rubani, katika eneo la Rubaya, wilayani Masisi. Afisa mmoja wa kidiplomasia na afisa mwengine mwandamizi wa kundi hilo la M23 wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa Willy Ngoma na maafisa wengine wa M23 walikuwa wakisafiri waliposhambuliwa na ndege hizo zisizo na rubani. #DiraYaDuniaTV