- 19,168 viewsDuration: 28:11Serikali ya Uganda iko chini ya shinikizo la kuingilia kati kesi ya mfanyakazi wa ndani anayekabiliwa na adhabu ya kifo nchini Syria. Shirika la habari la MMI News lenye makao yake Uingereza limenukuu shirika la Migrant Workers Voice Uganda likiwahimiza maafisa jijini Kampala kuzungumza na wenzao wa Syria ili kusimamisha utekelezaji wa hukumu hiyo dhidi ya Vicky Ajok ambayo imepangwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii tarehe 28 Februari. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw