- 2,190 viewsDuration: 1:38Viongozi wa Kenya Kwanza Kutoka Jamii ya Kipsigis wamemkashifu Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa matamshi yake kwamba Jamii ya Kalenjin haina Kiongozi anayezungumza kwa niaba ya jamii hiyo. Viongozi hao wakiongozwa na kiongozi wa wengi katika bunge la seneti Aaron Cheruiyot wamesema kwamba matamshi ya Gachagua hayana msingi na kwamba yanalenga tu kuleta Ubabe wa kisiasa Katika Jamii hiyo.