Mahakama yaongezea muda agizo la kusitisha msasa wa makatibu wateule

  • | Citizen TV
    1,460 views

    Agizo la mahakama kuhusu kusitishwa kwa msasa wa makatibu wateule litaendelea kutekelezwa hadi tarehe ishirini na tisa mwezi huu ambapo kesi hiyo itasikizwa. Jaji Nduma Nderi amekataa kuondoa makataa hayo na kuagiza kujumuishwa kwa kesi zingine mbili zilizowasilishwa mahakamani kupinga uteuzi na msasa wa makatibu hao wateule. Bunge liliwasilisha kesi kudai kuwa mahakama ya ajira na leba haina mamlaka ya kusikiza kesi hizo na kusema kuwa iwapo suala hilo halitatatuliwa kabla ya siku 28 kukamilika, basi makatibu wateule wataapishwa na kuanza kazi. Mwanasheria mkuu pia aliwasilisha rufaa kupinga uamuzi wa mahakama uliositisha mahojiano ya makatibu wateule. Rufaa hiyo itasikizwa hapo kesho