- 124 viewsDuration: 5:07Ann Wambui Kimone anajulikana kama mlezi wa watoto wenye ulemavu kwenye shughuli ambayo alianza wakati wa janga la Corona. Ann ambaye ni mwalimu amekuwa matumaini kwa watoto wengi ambao wanamtegemea kwa masomo na mahitaji ya kimsingi katika eneo la Mowlem hapa Nairobi. Je ni kipi kilichomsukuma kuchukua jukumu zito la ulezi huu na kipi kinachompa nguvu ya kuendelea kila uchao?