Hussein Gufu aibuka mshindi kwenye shindano la InterswitchSPAK

  • | Citizen TV
    230 views

    Hussein Gufu ameibuka mshindi kwenye shindano la Interswitch ambalo limekuwa likipeperushwa na runinga ya citizen. Mshindi wa shindano hilo amepata ufadhili wa masomo wa shilingi 1.5m na kipakatalishi huku walioibuka wa pili na tatu wakipata Ksh 750,000 na Ksh 150,000 na kipakatalishi kila mmoja. Shindano hilo ambalo lilijumuisha mafunzo, teknolojia na burudani lilinuia kuwatambua na kuwakuza wanafunzi wanaoenzi masomo ya sayansi. mashindano hayo kwa jina InterswitchSPAK hufanyika kila mwaka na kuwashirikisha wanafunzi kutoka shule za upili za umma na za kibinafsi. shindano hilo hufanyika kwa ushirikiano na wizara ya elimu, na wadau wengine na huwashirikisha wanafunzi wa kidato cha tatu walio na umri wa kati ya miaka 15 na 18