- 649 viewsRais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi amemteua aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Jean-Pierre Bemba, ambaye alikuwa gerezani kwa zaidi ya miaka 10 kwa uhalifu wa kivita, kuwa waziri wa ulinzi wa nchi hiyo katika mabadiliko makubwa kwenye serikali. Uteuzi wake ulikuwa sehemu ya mabadiliko makubwa ya maafisa 57 wa serikali, ambayo msemaji wa rais alisema ni ya "haraka na lazima", katika tangazo kupitia kituo cha televisheni ya taifa ya Kongo. Rais huyo pia amemteua Vital Kamerhe, mkuu wake wa zamani wa utawala, ambaye aliachiliwa kutoka gerezani mwezi Desemba 2021 baada ya kupatikana na hatia ya ubadhirifu, wakati alipokuwa waziri wa Fedha. Kamerhe Juni mwaka 2022 alifutiwa mashtaka yote baada ya kukataa rufaa dhidi ya mashtaka hayo. Mabadiliko hayo, ambayo yalikuwa makubwa zaidi kuliko ilivyotabiriwa, yamekuja kabla ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Desemba 20, ambapo Tshisekedi anatarajiwa kuwania muhula wa pili. #felixtshisekedi #vitalkamerhe #JeanPierreBemba #drc #mawaziri #uteuzi #congo #voa #voaswahili #dunianileo #rais - - - - - #VOASwahili - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.
Raia wa DRC atoa maoni yake juu ya uteuzi wa Bemba na Kamerhe
- 29 Apr 2024 - Roads and Transport Cabinet Secretary (CS) Kipchumba Murkomen has pleaded with Kenyans to heed all safety directives issued by the national and county governments on the ongoing floods to avert further loss of lives.
- 29 Apr 2024 - Several people are feared dead after an improvised explosive device (IED) detonated at the centre of Elwak town, Mandera County on Monday.
- 29 Apr 2024 - Several people are feared dead after an improvised explosive device (IED) detonated at the centre of Elwak town Marsabit County on Monday.
- 29 Apr 2024 - African leaders on Monday called for rich countries to commit record contributions to a low-interest World Bank facility for developing nations that they rely on to help fund their development and combat climate change.
- 29 Apr 2024 - Nairobi Governor Johnson Sakaja now says that his administration will give priority to residents of Nairobi City Council (Kanjo) estates when the affordable houses are ready.
- 29 Apr 2024 - Embattled Bomas of Kenya CEO Peter Gitaa has pleaded not guilty to eight counts of failure to comply with procurement laws.
- 29 Apr 2024 - The directive followed the postponement of the schools' opening date.
- 29 Apr 2024 - Motorists plying the Mai Mahiu-Suswa/Narok highway and the Mai Mahiu - Naivasha road have been advised to look for alternative routes after debris was swept into the roads following Sunday night's heavy downpour.
- 29 Apr 2024 - In March 2024, the Ethics and Anti-Corruption Commission (EACC) released its corruption index survey, in which KEBS was identified as one of the top three most corrupt public entities.
- 29 Apr 2024 - Mathare Member of Parliament (MP) Anthony Oluoch urged President William Ruto to address the flood situation in the country and declare it a national disaster.