Viongozi wa Kenya Kwanza washutumu maandamano Azimio

  • | K24 Video
    250 views

    Naibu Rais Rigathi Gachagua ameiomba jamii ya kimataifa impuuze kinara wa muungano wa Azimio Raila Odinga, kufuatia wito wake Raila kwa jamii hiyo kuhusiana na kupigania demokrasia. Gachagua vilevile amewaonya vikali wale wanaojihusisha na uhalifu wakati wa maandamano. Waziri wa uchukuzi kipchumba Murkomen vilevile amesisitiza kuwa uharibifu unaofanyika barabarani wakati wa maandamano utagharimikiwa na vyama binafsi vilivyo ndani ya muungano wa Azimio.