Wafanyikazi wa umma walalamikia makato

  • | Citizen TV
    816 views

    Wafanyikazi wa umma sasa wanaitaka serikali kusistisha malipo kwa hazina ya uzeeni - NSSF, wakisema kuwa tayari walikuwa wakitozwa malipo ya kustaafu kupitia hazina ya uwekezaji ya kustaafu kupitia kwa mwajiri wao. Wafanyikazi hao wamekatwa asilimia sita ya mishahara yao ya mwezi Julai kwa mujibu wa sheria mpya ya NSSF. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, wafanyikazi hao wamelalamikia gharama ya juu ya maisha na kuirai serikali kuwapa nyongeza ya mshahara badala ya kuongeza kodi wanayokatwa kwa sasa.