Omtatah kukata rufaa katika Makahaka ya Upeo

  • | Citizen TV
    945 views

    seneta wa busia Okiya Omtatah na watu wengine wanne wametoa ilani ya kuwasilisha rufaa katika makahaka ya upeo kupinga uamuzi wa mahakama ya rufaa ulioidhinisha utekelezaji wa sheria ya fedha. Omtatah, eliud karanja matindi, benson odiwor otieno na blair ongima oigoro wanasema kuwa hawajaridhishwa na uamuzi wa mahakama ya rufaa kuhusu sheria ya fedha ya mwaka 2023/24, uliotolewa na majaji Mohammed Warsame, Kathurima M’Inoti na Hellen Omondi. majajihao waliweka kando uamuzi wa awali wa mahakama kuu wakisema kuwa wameridhishwa na kauli ya serikali kuwa imekuwa ikipoteza zaidi ya shilingi nusu bilioni kila siku ambayo sheria ya fedha haitekelezwi.