Muungano wa Azimio One Kenya waendeleza kampeni katika kaunti ya Makueni

  • | K24 Video
    109 views

    Muungano wa Azimio One Kenya umetupilia mbali madai kuwa huenda kutakuwa na wizi wa kura kama inavyodaiwa na muungano wa Kenya Kwanza. Akihutubia wakazi katika mkutano wa kampeni huko Makueni, mgombea urais Raila Odinga amekashifu Kenya Kwanza kwa kuibua madai hayo akisema Ruto amejawa na uoga wa kupambana naye Agosti 9. Katika kampeini hiyo Raila aliahidi kutafuta suluhu ya kudumu ya uhaba wa maji na baa la njaa katika eneo hilo.