Makanisa ya Kimethodisti yaunga mkono udhibiti wa maabadi

  • | Citizen TV
    555 views

    Muungano wa makanisa ya Kimethodisti nchini umeunga mkono hatua ya serikali kudhibiti baadhi ya makanisa yanayoendeleza itikadi potofu za kidini. Askofu mkuu wa makanisa hayo Afrika Mashariki Daniel Wandabula amesema kuna haja ya viongozi wa makanisa kudhibitiwa ili kuhakikisha taalauma hiyo haitumiwi vibaya. Wandabula alizungumza kaunti ya Mombasa, wakati wa mkutano uliojumuisha wawakilishi kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika Mashariki.