Aliyekuwa kiongozi wa wengi katika bunge la kaunti ya Nyamira Elijah Osiemo azikwa

  • | Citizen TV
    770 views

    Familia, marafiki na viongozi wa kisiasa wamemtaja marehemu Elijah Osiemo ambaye alikuwa mwakilishi wadi wa Nyamaiya na kiongozi wa walio wengi katika kaunti ya Nyamira kama kiongozi aliyekuwa na maono mazuri kwa eneo la Nyamaiya. Familia ya marehemu imeomba asasi za usalama kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini hali halisi kuhusu ajali iliyosababisha kifo chake osiemo. Osiemo aliaga dunia kwenye ajali ya barabarani katika eneo la Naivasha alipokuwa safarini kwenda kwenye mkutano wa kamati maalum kabla ya gari lao kugongana na pikipiki. Osiemo amemwacha mjane na watoto watatu.