Naibu rais Rigathi Gachagua awataka wanabodaboda kuwajibika

  • | Citizen TV
    1,407 views

    Naibu Rais Rigathi Gachagua amewataka waendeshaji bodaboda kuhakikisha kuwa sekta hiyo haingiliwi na wahalifu wanaojifanya kuwa wafanyibiashara. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango wa kutoka mafunzo wa Boda Yangu Ofisi Yangu, Gachagua aliwaonya waendeshaji bodaboda dhidi ya jaribio la kuruhusu magenge ya wahalifu haswa katika eneo la Mlima Kenya kuingilia Shughuli zao. Aidha aliwataka wahudumu wa bodaboda waheshimu sheria huku akisema polisi wamehimizwa kushirikiana nao kuhakikisha shughuli zinaendelea kama zinavyofaa Mpango huo wa mafunzo unafadhiliwa na mwakilishi wa kike wa kaunti Nyandarua Faith Gitau, chini ya hazina ya serikali ya jinsia. Waendeshaji bodaboda 256 watapokea mafunzo kuhusu jinsi ya kuweka akiba mbali na usalama barabarani na pia kujiunga na hazina ya matibabu NHIF.