Washukiwa wa ulanguzi wa watoto katika hospitali ya Mama Lucy kuzuiliwa magerezani

  • | K24 Video
    66 views

    Washukiwa wawili wa ulanguzi wa watoto uliotokea miaka mitatu iliyopita katika hospitali ya Mama Lucy watazuiliwa katika magereza ya Industrial area na lile la wanawake la Lang'ata. Wawili hao Selina Adundo na Fred Leparan walikuwa wahudumu wa afya ya jamii. Haya yanajiri huku hakimu mkuu katika kesi inayomkabili aliyekuwa gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya akiagiza upande wa mashtaka na mawakili wanaomwakilisha Oparanya wafanye kikao cha pamoja na kuafikiana kuhusu stakabadhi zinazofaa kwa kesi hiyo ili zihifadhiwe.