Baadhi ya wakulima Nandi waipa serikali ardhi ili kuwesha ukuzaji wa chakula

  • | Citizen TV
    951 views

    Baadhi ya wakulima kaunti ya Nandi wametoa ardhi yao na kuipokeza serikali ili kuwesha ukuzaji wa chakula kitakachopelekewa wakazi wa maeneo yanayokabiliwa na ukame na uhaba wa chakula. wakulima hao wanasema hatua hiyo itahakikisha kuwa wakenya wenzao hawafi njaa, wakitumai itakuwa kielelezo kwa jamii zingine zinazoishi katika maeneo yanayokuza chakula. aidha wakulima hao wameamua kuchanga mahindi waliyovuna mwaka huu kuwasaidia wakazi wa kaskazini mwa nchi.