Marufuku ya buibui Ufaransa

  • | Citizen TV
    1,142 views

    Wafaransa wamegawanyika kuhusu marufuku ya vazi la buibui au kanzu katika shule za sekondari baada ya amri ya Waziri wa elimu kuanza kutekelezwa jumatatu hii kwenye siku ya kwanza ya msimu mpya wa masomo nchini humo. Serikali inadai inatekeleza sheria ya mwaka wa 1905 ya kutenganisha masuala ya dini na serikali, huku wafaransa wengi hasa waislamu wakisema ni uwonevu na ubaguzi wakitoa hoja kwamba mavazi hayo si alama za uislamu.