Jopo la vyama lasitisha juhudi za kuwatimua wabunge wa ODM waliofurushwa chamani

  • | Citizen TV
    156 views

    Imekuwa afueni kwa wabunge watano wa chama cha ODM baada ya jopo la kusikiliza mizozo ya vyama kutoa agizo kuzuia kutimuliwa kwao. Agizo hili likifuatia ombi la seneta wa Kisumu Tom Ojienda, mbunge wa Gem Elisha Odhiambo na mbunge wa Lang'ata Phelix Odiwuor wakisubiri uamuzi wa jopo hili. Odm mapema mwezi huu iliafiki kuwatimua wabunge hawa pamoja na mbunge wa Suba South Caroli Omondi na mwenzake wa Uriri Mark Nyamita