Utafiti wa Infotrak unaashirikia kuwa asilimia 53 ya Wakenya wanahisi Kenya haiendeshwi sawa

  • | Citizen TV
    98 views

    Utafiti wa punde wa kampuni ya Infotrak unaashirikia kuwa asilimia 53 ya Wakenya wanahisi kuwa taifa la Kenya haliendeshwi kwa njia ya kuridhisha. Aidha, Utafiti huu uliotolewa hii leo umeratibu gharama ya juu maisha na ukosefu wa ajira kama masuala ambayo Wakenya wanalalamikia kuyahusu, mwaka mmoja baada ya serikali ya Kenya Kwanza kuingia mamlakani. Utafiti huu pia ukionyesha kuwa asilimia 55 wana imani na uongozi wa Rais William Ruto huku 47 wakiwa na imani na majukumu ambayo yamekua yakitekelezwa na naibu rais Rigathi Gachagua. Kuhusu utendakazi wa mawaziri, waziri Kindiki Kithure ametajwa kuwa bora