Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akutana na Rais wa Kenya William Ruto

  • | VOA Swahili
    413 views
    Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amekutana na Rais wa Kenya William Ruto mjini New York Alhamisi pembeni ya kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Ruto ameweka nia ya dhati kuwa nchi yake itaongoza kikosi cha kimataifa nchini Haiti kupambana na magenge yenye silaha ya kivita licha ya wakazi wa nchi zote hizo mbili kudadisi mpango huo unaosukumwa na serikali ya Marekani. Marekani imeipongeza Kenya kwa kufikiria kuongoza kikosi kinacho ungwa mkono na Umoja wa Mataifa wakati nchi nyingine zimesita, na Marekani inaandika rasimu ya azimio la Baraza la Usalama la UN kuruhusu kikosi hicho kupelekwa Haiti. -AP #rais #kenya #waziri #mamboyanje #antonyblinken #williamruto #haiti #kikosichakimataifa #magenge #voa #voaswahili #unga #barazalausalama - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.