Mwalimu ampiga na kumjeruhi mwanafunzi wa kidato cha nne shuleni Sacred Hill Londiani

  • | Citizen TV
    2,960 views

    Maafisa wa polisi katika eneo la Londiani kaunti ya Kericho wanachunguza kisa ambapo mwanafunzi wa shule ya upili ya wasichana ya Sacred Hill, Londiani anadai kujeruhiwa na mwalimu. Mwanafunzi huyo anadai kuchapwa siku ya jumatatu na mwalimu mkuu na kisha kutimuliwa shuleni bila wazazi wake kujulishwa. Aliporejeshwa shuleni siku ya alhamisi na mzazi inadaiwa kwamba usimamizi wa shule uliwaita maafisa wa polisi ambapo mama na mwanawe walikamatwa.