- 271 viewsDuration: 3:10Wakulima wa mifugo katika Kaunti ya Murang’a sasa wanageukia kilimo cha miti ya malisho ya mifugo inayofahamika kama Trichanthera. Hii ni katika juhudi za kujihakikishia lishe ya kutosha kwa mifugo wao kwa gharama nafuu. Mmea huu ambao asili yake ni Amerika Kusini, sasa unatajwa kama suluhisho kwa kuongeza mazao ya maziwa huku wakulima wakipunguziwa gharama ya kununua lishe dukani. Denis Otieno anaarifu kwenye makala ya Kilimo Biashara.