Skip to main content
Skip to main content

'Lissu kutofika mahakamani leo kwa sababu za kiusalama'

  • | BBC Swahili
    43,709 views
    Duration: 37s
    Mahakama kuu ya Tanzania masijala ndogo ya Dar es salaam imeamuru mshtakiwa wa kesi ya uhaini Tundu Lissu ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha upinzani CHADEMA kufikishwa mahakamani hapo tarehe 12/11/2025 siku ya Jumatano Hii leo Jumatatu tarehe 10/11/2025 hakufikishwa mahakamani kwa kile upande wa waleta mashitaka (Jamuhuri) kudai hajafikishwa mahakamani kutokana na hali ya kiusalama katika Jiji la Dar es salaam baada ya ghasia za uchaguzi, - Mashahidi wa Lissu na wa Jamuhuri nao pia hawakufika mahakamani kwa sababu hizo hizo na mahakama imeamuru wajiandae na wafike mahakamani siku iliyoelekezwa ili kuweza kuendelea na shauri hilo - - #bbcswahili #lissu #siasa #uchaguzi2025 Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw