Mwanasheria Mkuu Justin Muturi ataka majukumu yatengwe na tume ya PSC

  • | KBC Video
    97 views

    Mkuu wa sheria Justin Muturi anapendekeza marekebisho kuiwezesha afisi yake kutekeleza wajibu wake bila mwingilio wa tume ya utumishi wa umma. Muturi aliyefika mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu haki na masuala ya sheria anapendekeza marekebisho kupitia mswada wa marekebisho ya sheria ili kubuniwe bodi katika afisi ya sheria ya serikali itakayosimamia ajira, upandishwaji vyeo pamoja na kushughulikia masuala ya nidhamu ya wafanyakazi. Katika uwasilishaji wake, Muturi amesema hatua hii itasuluhisha changamoto za kuwepo kwa uhaba wa wafanyakazi, malipo na urasimu. Fauka ya hayo, alitupilia mbali madai ya vyombo vya habari kwamba afisi yake ina utepetevu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive