- 30,869 viewsDuration: 2:22Mpasuko ndani ya muungano wa upinzani umeendelea huku vigogo wa mrengo huo wakiongozwa na kinara wa chama cha DCP Rigathi Gachagua wakiongoza mashambulizi dhidi ya chama cha Jubilee kinachoongozwa na rais mstaafu Uhuru Kenyatta. Katibu mkuu wa jubilee Jeremiah Kioni aidha, akimkashifu Gachagua kwa kugawanya upinzani, akidai anashirikiana na rais William Ruto akiwahadaa tu wakenya.