- 721 viewsDuration: 3:36Eneo la Tuwan, viungani mwa mji wa Kitale, mara nyingi limekuwa likitajwa kwa visa vya utovu wa usalama. Lakini maisha ya Mirel Atieno, askari wa kaunti au Kanjo, yanabadilisha taswira ya eneo hilo. Mirel, ambaye amevunja vikwazo na kuwapiku warembo wengine humu nchini, sasa anajiandaa kuiwakilisha Kenya kwenye mashindano ya kimataifa ya Miss Earth yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao nchini Ufilipino