Skip to main content
Skip to main content

Wahadhiri na wafanyakazi wa vyuo vikuu waapa kuendelea na mgomo

  • | KBC Video
    3,855 views
    Duration: 4:01
    Masomo katika vyuo vikuu vya umma yametatizika kwa wiki ya tatu mfululizo, huku wahadhiri wakiapa kuendelea na mgomo hadi serikali itakapowalipa shilingi bilioni 7.9 kuambatana na mkataba wa makubaliano wa mwaka wa 2017. Wakihutubia wanahabari jijini Nairobi, viongozi wa chama cha wahadhiri wa vyuo vikuu UASU na chama cha wafanyakazi wa vyuo vikuu KUSU walipinga madai ya tume ya uratibu wa mishahara SRC kwamba serikali ina deni lao la shilingi milioni 624 pekee. Naye waziri wa elimu Julius Ogamba aliyefika mbele ya kamati ya elimu ya bunge la Seneti, alisema upo mtafaruku baada ya tume ya uratibu wa mishahara kuashiria kwamba shilingi bilioni 7.2 kati ya bilioni 7.9 zilikuwa zimelipwa. Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/ #kbcchannel1 #news #kbclive