Chama cha wauguzi cha KNUN kimekashifu shambulizi dhidi ya wauguzi wanaogoma katika kaunti ya Siaya, kikidai serikali ya kaunti hiyo ilitumia wahuni kuwatishia wafanyikazi hao wanaogoma. Katibu mkuu wa chama hicho, Seth Panyako, amesema wauguzi hao hawatayumbishwa na vitisho, akionya kwamba matakwa yao sharti yatimizwe na serikali ya kaunti ya Siaya kabla ya kurejea kazini. Maafisa wa KNUN, tawi la Siaya wamesema wauguzi 20 walijeruhiwa wakati wa vurugu hiyo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive