Chama cha wamiliki wa mabaa, hoteli na maduka ya kuuza vileo pamoja na kile cha wauzaji rejareja wamewasilisha ombi kwenye bunge la seneti ili kusitisha mjadala kuhusiana na mswada wa marekebisho ya sheria ya kudhibiti tumbaku wa mwaka 2024. Vyama vyote viwili vinadai kuwa mswada huo uliwasilishwa kwenye bunge hilo bila ushirikishwaji ufaao wa umma, na mapendekezo yake iwapo yatakubaliwa yataibua biashara haramu badala ya kupunguza vifo pamoja na madhara yanayosababishwa na matumizi ya sigara.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive