Shughuli za usafiri katika barabara ya Lamu-Garsen zakatizwa baada ya mafuriko kuharibu barabara

  • | Citizen TV
    1,696 views

    Shughuli za usafiri katika barabara ya Lamu - Garsen bado zimekatizwa, baada ya mafuriko kuharibu barabara hiyo katika eneo la Gamba. Mamia ya wasafiri sasa wanalazimika kugharamika zaidi kwa kutumia mashua kuvuka eneo lililoharibika, huku wanafanyabiashara wakikadiria hasara kutokana na ongezeko la nauli na bei ya kusafirisha bidhaa zao. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, serikali ya kaunti ya Lamu sasa imetoa wito kwa mamlaka ya ujenzi wa barabara kuingilia kati ili kurejesha shughuli za usafiri katika barabara hiyo.