Katika hali isiyo ya kawaida, wafanyakazi waliogoma katika chuo kikuu cha kilimo na teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) walibadili ratiba yao ya kawaida na kutumia siku yao wakifurahia michezo na burudani. Wakiongozwa na viongozi wa chama cha wahadhiri wa vyuo vikuu (UASU) na chama cha wafanyakazi wa vyuo vikuu (KUSU), katika chuo hicho, wahadhiri ambao hawajakuwa darasani kwa kipindi cha majuma manne, walisitisha shinikizo zao za kudai mishahara, na wakashiriki mbio na michezo mingine ya kujifurahisha.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive