Rais ageuza nia kuhusu ujenzi wa ghorofa Eastleigh

  • | Citizen TV
    6,328 views

    Rais William Ruto amebadilisha msimamo wake kuhusu sheria zinazodhibiti urefu wa majengo karibu na Kambi ya Jeshi la Wanahewa ya Moi Airbase mtaani Eastleigh jijini Nairobi .Hatua hii imejiri kufuatia wasiwasi kwamba majengo marefu huenda yakatumika kama ngome ya maadui. Hata hivyo, Rais ameugeuza msimamo wake mwezi mmoja tu baada ya kuamuru kuondolewa kwa amri iliyokuwa inazuia ujenzi wa majengo yenye ghorofa zaidi ya 12 karibu na kambi ya jeshi. Serfine Achieng’ Ouma ana maelezo zaidi.