Maelfu ya vijana wajumuika katika uwanja wa Uhuru Park kuwakumbuka waliouawa na polisi

  • | Citizen TV
    6,371 views

    Maelfu ya vijana leo wamejumuika katika uwanja wa Uhuru Park hapa Nairobi, lwa hafla ya kuwakumbuka zaidi ya watu 40 waliouwawa wakati wa maandamano ya kupinga serikali. Hafla hiyo iliyohudhuriwa na zaidi ya wasanii 30 tajika nchini, ilijumuisha vijana wa tabaka mbalimbali na hata familia za waliowapoteza wapendwa wao kwenye maandamano hayo. Emmanuel Too alikuwepo na hii hapa taarifa yake