Mahakama ya leba yasitisha kwa muda mgomo wa walimu kote nchini

  • | K24 Video
    12 views

    Mahakama ya leba imesitisha kwa muda mgomo wa walimu kote nchini. hii ni baada ya tume ya kuajiri walimu ,TSC, kuwasilisha kesi dhidi ya chama cha walimu wa shule za upili , KUPPET. Hayo yakijiri , viongozi wa KUPPET wameapa kuendelea na mgomo wakisema kuwa bado hawajapokea rasmi agizo la mahakama. viongozi hao wanadai agizo hilo sasa limechochea mgomo ulioingia siku ya pili uendelee. Kinachowatamausha walimu ni msimamo wa wizara ya elimu wa kuzidi kufanya mazungumzo nao ili kutatua masuala yao ila sasa wanalazimishwa kushika chaki kimabavu.