'Kufa makanga... Kufa dereva!'

  • | Citizen TV
    4,515 views

    Zoezi la kukusanya maoni kuhusu kubanduliwa kwa naibu rais Rigathi Gachagua limeanza leo sehemu nyingi nchini huku idadi kubwa ya wakenya sasa wakimtaka Rais William Ruto kuondolewa ofisini pamoja na naibu wake. Wakenya hawa waliozungumza kwenye vikao vya umma vilivyoanza katika kaunti zote nchini wamesema utakuwa ni unafiki mkubwa endapo Gachagua atabanduliwa ofisini peke yake bila ya Rais aliyechaguliwa naye.