
38,002 views
2 Oct 2026
STANZA 1 Zitaonyeshwa kanzu na nguo zipi ukitoweka ndugu, kusanyiko lipi litajumuika, maneno yepi atasemwa kwako. Kama Tabitha mwanafunzi wa Mungu wahudumie wenye hitaji, wajane, mayatima, wagonjwa, masikini uwafikie wote. CHORUS Akiwapo nduguzo masikini ndani ya malango yako, usifanye mgumu moyo wako, usimfumbie mkono wako. Mkopeshe yatoshayo haja yake, na wala usisikitike utakapompa lisiwe neno lisilofaa moyoni mwako. STANZA 2 Kadiri ulivyoipokea karama, vile vile itumie. Fanya haraka nafasi yako sasa, usiku waja hutaweza kazi. Kwa kujinyima na kujitolea ndugu, kwa uwezo na kwa Sala zako. Mmepokea bure nanyi toeni bure, mkristo sambaza upendo.