
272,027 views
23 Jan 2026
STANZA 1 Wakashikwa na tamaa wana wa Israeli, Samaki tulokula bure kule misiri, twataka matango matikiti twataka, (tupe Musa tule×2). Tulikuwa na uheri misiri, sasa twala mana kama chembe za mtama. Hasira za bwana zikawaka, malalamiko yao yalizidi CHORUS [Kibroth hataava] makaburini walikozikwa [wenye manung’uniko]wepesi wa kusahau, wakatafuta kosa pasipo kosa, halikuwatoka jasho wapate mana, ilivyowagharimu huduma ngumu misiri, mwanadamu jichunguze, malalamiko yako yatakukosesha mbingu mpya STANZA 2 Mbona wahangaika, mbona unagombana, ingawa hali yako ndugu nzuri zaidi, Mungu amekugawa zaidi ya wengine, (mbona walalama x2) utawala wa hisia za mwili hupotosha mtazamo kwa yanayodumu, jifunze kuridhika na yale uliyopewa, tena ushukuru