- 294 viewsDuration: 3:31Afisa mkuu wa mamlaka ya afya ya jamii - SHA - , Dkt. Mercy Mwangangi amesema kuwa mamlaka hiyo ilirithi deni la shilingi bilioni 33 kutoka kwa NHIF. Akihojiwa na kamati ya uwekezaji , mwangangi amesema kuwa bado deni hilo linathibitishwa kabla ya malipo kutolewa. aidha mwenyekiti wa kamati hiyo Caleb Amisi, ameibua masuali kuhusu uhamisho wa shilingi bilioni 15 za NHIF kwa SHA,ambazo zimetajwa na mhasibu mkuu wa serikali kama kinyume na sheria.