- 5,837 viewsDuration: 2:59Jioni ya leo, familia nyingine inadai maelezo zaidi kutoka kwa serikali kufuatia ripoti kuwa jamaa yao amefariki akipigana vita nchini Urusi. Familia ya Peter Maina Gakau ikidai kuwa jamaa yao alichukua likizo kutoka kazini katika kitengo cha GSU kuelekea Urusi kwa kazi ya muda. Ode Francis anaarifu huku familia zaidi zikiendelea kujitokeza kuhusu jamaa zao waliosafiri Urusi baada ya serikali kukiri wakenya zaidi ya elfu moja walisafiri nchini humo.